Wednesday, May 05, 2010
AL-SHAYMAA, KIMAYA WATANGAZA NIA KUWANIA UBUNGE MBELE YA WAZIRI MKUU
MBUNGE wa Kuteuliwa na Rais, Bi. Al-Shaymar John Kwegyir na Mwenyekiti wa Chama cha Watu Wenye Ulemavu wa Ngozi Tanzania, Bw. Ernest Kimaya ambao wote ni walemavu wa ngozi wametangaza nia ya kugombea ubunge katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba, mwaka huu.
Akizungumza na wakazi wa mji wa Iringa, leo mchana (Jumanne, Mei 04, 2010) wakati wa maadhimisho ya Siku ya Walemavu wa Ngozi Tanzania yaliyofanyika kwenye viwanja vya Garden mjini humo, Bw. Kimaya amesema ana nia ya kugombea ubunge jimbo la Korogwe Vijijini kwa tiketi ya CCM.
Alisema amefikia uamuzi huo ili kitimiza kauli mbiu ya mwaka huu ambayo inawahimiza wajitokeze kugombea. Kaulimbiu ya mwaka huu inasema: “Uchaguzi wa Serikali, Mlemavu wa Ngozi ana Haki ya Kuchagua na Kuchaguliwa, Tujitokeze”.
Akihutubia wakazi hao, Waziri Mkuu Mizengo Pinda alisema amedokezwa na mbunge Kwegyir kwamba ana nia ya kwenda kugombea viti maalum mkoa wa Tanga. “Anasema anamshukuru Rais Kikwete kumteua katika ubunge na sasa anataka aende viti maalum,” alisema Waziri Mkuu.
“Napenda kutoa wito kwa wananchi wote wakiwemo watu wenye Ulemavu wa Ngozi nchini kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali kupitia vyama vyao vya siasa, mnayo fursa ya kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kama ilivyo kwa wananchi wengine. Jitokezeni pia kwenye zoezi zima la upigaji kura. Wote mnayo haki ya msingi kushiriki kikamilifu katika zoezi hili kama ilivyo kwa Watanzania wote,” alisema.
Aliwataka Watanzania watambue kuwa watu wenye ulemavu wa ngozi wana mchango mkubwa katika jamii hasa wakiwezeshwa na binadamu wenzao wasio na ulemavu huo. “Wito wangu kwa jamii ya Watanzania ni kuwa Iwape Nafasi Kwani Wanaweza,” alisema.
Maadhimisho hayo pia yalihudhuriwa wa wawakilishi wa watu wenye ulemavu kutoka mikoa zaidi 15, Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Aisha Kigoda; Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Bw. Mohammed Abdulaziz; Mbunge Kwegyir; Bi. Margareth Mkanga na wabunge wengine kutoka mkoa wa Iringa.