Friday, May 21, 2010
KILIMO CHA JEMBE LA MKONO SASA BASI - PINDA
Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda amesema Kilimo cha Jembe la Mkono Nchini sasa basi kwa vile kimeshindwa kuleta Mapinduzi ya Kilimo na badala yake lazima kutumia zana za Kisasa na Utalaamu.
Alikuwa akihutubia Mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Mirumba, Kata ya Kibaoni, Tarafa ya Mpimbwe baada ya kukabidhi Matrekta kwa vikundi vya Wakulima katika siku yake ya nne ya ziara yake ya Jimbo.
“Jembe la Mkono siyo zana ya kutegemea kubadili maisha yetu… Wenzetu wanalima kwa Matrekata madogo na makubwa, wanapanda na kuvuna kwa Matrekta… Majembe ya Mkono yalitumika zaidi ya Miaka 2000 iliyopita” alisema.
Alikabidhi Trekta moja kubwa kwa kikundi cha Mbugani cha Kijiji cha Itenka; moja dogo kwa kikundi cha Jitume cha Kijiji cha Magamba na jingine dogo kwa kikundi cha Ufugaji Nyuki cha Kijiji cha Uruira.
Trekta kubwa aina ya Tafe, liliotengenezwa India, lina thamani ya Shilingi Milioni 51 na Wakulima wanatakiwa kuilipa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Shilingi Milioni 10 ambayo ni Asilimia 20 ya gharama Halmashauri hiyo iliingia kulinunua.
Trekta dogo aina ya Kubota la Japan Wakulima hutakiwa kulipia Shilingi Milioni 1.5, ikiwa ni Asilimia 10 tu ya bei yake.
Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda tangu mwaka 2007/2008 imekuwa ikitekeleza agizo la Serikali la kununua Matrekta na kuyasambaza kwa Wakulima kwa bei ya chini, ikiwa ni sehemu ya kuendeleza Kilimo cha zana na cha Kisasa.
Kwa mwaka huu wa fedha unaomalizika Mwezi ujao (2009/2010), Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda ilipanga kununua Matrekta madogo 36, kwa gharama ya Shilingi Milioni 284 na Matrekta makubwa matano ya Shilingi Milioni 258, ikiwa ni utekelezaji wa Mpango huo.
Matrekta madogo 11 yaliyogharmu Shilingi Milioni 78 yaligawiwa kwa vikundi 11 vya Tarafa za Nsimbo, Karema, Mpimbwe na Kabungu, kwa mwaka 2008/2009.
Trekta kubwa kwa saa 8 kwa kutwa hulima kiasi cha ekati 10 na dogo ekari 5 wakati kwa Mkono, kwa Mkulima mmoja hata eka moja haiwezekani kuilima kwa kutwa nzima, kwa mujibu wa Wataalamu.
Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda pia imenunua Mashine ya Kisasa ya kukobolea Mpunga na kuupanga Mchele kwa Madaraja, kwa gharama ya Shilingi Milioni 250 ili kuongeza thamani ya zao hilo na kuongeza pato la Mkulima.
Mashine hiyo ya kutoa Mchele, itawekwa katika Kijiji cha Mwamapuli kwenye Soko kubwa la Kisasa lililojengwa na Halmashauri kuptia mpango wake maendeleo wa Wilaya kuwaendeleza Wakulima.
Mheshimiwa Pinda pia alikabidhiwa michango ya Wananchi mbalimbali waliojitolea kumlipia fomu ya kugombea Ubunge kupitia kwa Chama chake cha CCM, uliofikia Shilingi 305,000/= katika Kijiji cha Mirumba; Shilingi zaidi ya 102,300/=, katika Kijiji cha Itenka ‘B’ (zikiwemo 2,000/=) zilizochangwa na Mlemavu na Shilingi 300/= za Mtoto wa Shule) na Shilingi 10,000/= katika Kijiji cha Kasansa.
Gharama za fomu ni Shilingi 100,000/= na Mheshimiwa Pinda alizikabidhi fedha zilizosalia kwa CCM, Wilaya ya Mpanda kwa matumizi ya CCM na Jumuiya zake kwa shughuli za Kichama.
Kabla ya kuwasili Mpanda Mjini leo (Jumanne Mei 11, 2010) Waziri Mkuualitembelea Kijiji cha Itenka B na kuzungumza na Wananchi katika Mkutano wa hadhara.
Jana (Jumatatu Mei 10, 2010), alitembelea Kasansa, Kanindi ambako alikuwa na mikutano ya hadhara na kuhimiza Kilimo na akatembelea Majimoto ambako alikagua Jengo la Kisasa la SACCOS (Chama cha Kuweka na Kukopa) ya Majimoto, ambayo ni Makao Makuu ya Kata ya Majimoto katika Tarafa ya Mpimbwe.
Waziri Mkuu aliwasili Mpanda Jumamosi (Mei 8, 2010) na Jumapili akazungumza na Wananchi wa Kijiji cha Kibaoni, waliokubaliana kuanzisha Kilimo cha bega kwa bega kwa kutumia Trekta kubwa.
Kesho (Jumatano Mei 12, 2010) atatembelea Kamsisi na Mtakuja ambako atakuwa na Mkutano wa hadhara.
Anatarajiwa kurejea Dar es Salaam Mei 18, 2010 baada ya ziara yake ya Jimbo.