Monday, April 26, 2010

 

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Rais na muasisi wa Under The Same Sun, Peter Ash kutoka Canada ambaye ni albino kabla ya mazungumzo yao kwenye makazi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Aprili 26, 2010.

 

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akihutubia wakati alipofungua kongamano la Makatibu Muhtasi kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango Mjini DOdoma, Aprili 24, 2010.

 

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizindua Mkataba wa Huduma kwa Mteja baada ya kufungua Kongamano la Makatibu Muhtasi kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango Mjini Dodoma Aprili 24, 2010. Kulia kwake ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Celina Kombani, na Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ndugu Eliakim Maswi.

 

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na baadhi Makatibu Muhtasi kabla ya kufungua Kongamano lao kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango Mjini Dodoma, Aprili 24, 2010 Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Celina Kombani.

Friday, April 23, 2010

 

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina wakitoka kwenye ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma Aprili 23, 2010.

 

Katibu Mkuu Mstaafu, Rose Lugembe (kulia) akizungumza na Mbunge wa Lushoto, Balozi Abdi Mshangama kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Apili 23, 2010.

 

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Karani wa Baraza la Mawaziri, HAB Mkwizu kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Aprili 23, 2010.

 

9879 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Celina Kombani akiwa katika picha ya pamoja na wanawake kutoka Igunga , Tabora kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Aprili 23, 2010. Wanawake hao walialikwa na Mbunge wa Viti Maalum, Aziza Sleyum Ally (kulia kwa Waziri ) na kushoto ni Mbunge wa Sikonge, Said Juma Nkumba

Thursday, April 22, 2010

 

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja (kulia) na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Adam Malima wakitoka nje ya ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma, Aprili 22, 2010.

 

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dr. Hussein Mwinyi kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Aprili 22, 2010

 

Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Dk. Mary Nagu, akiwa Bungeni Mjini Dodoma Aprili 22, 2010

 

Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa (kushoto ) akiteta na Mbuge wa Mbarali, Estherina Kilasi, Bungeni Mjini Dodoma, Aprili 22, 2010.

 

Mbunge wa Bariadi Mashariki, John Cheyo akifuatilia mjadala wa muswada wa sheria ya madini, Bungeni Mjini Dodoma, Aprili 22, 2010

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mohamed Seif Khatibu (kulia) akiteta na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dr. Aisha Kigoda, Bungeni Mjini Dodoma Aprili 22,2010

 

Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja akisoma Muswada wa Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 . Bungeni Mjini Dodoma Aprili 20, 2010.

 

Waziri wa Mambo ya Ndani na Mbunge wa Nyamagana, Lawrence Masha (kushoto) akiteta na Naibu wa Wizara hiyo, Balozi Hamisi Kagasheki Bungeni Mjini Dodoma Aprili 22,2010.

 

Waziri wa Miundombinu, Dk Shukuru Kawambwa akisoma Bungeni taarifa ya serikali Aprili 22, 2010 kuhusu maendeleo ya ukarabati wa Reli ya kati unaotarajiwa kukamilika Mei 2010.

 

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid, Bungeni Mjini Dodoma, Aprili 22, 2010

 

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Mbunge wa Nachingwea na Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe, Bungeni Mjini Dodoma Aprili 22.2010

 

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akijibu Maswali, Bungeni Mjini Dodoma, Aprili 22, 2010.

 

Spika wa Bunge Samuel Sitta akiongoza kikao cha Bunge Mjini Dodoma Aprili 22, 2010.

 

Spika wa Bunge, Samuel Sitta akiongozwa na wapambe kuingia Bungeni, Aprili 22, 2010.

 

Wabunge Abdallah Sumry wa Mpanda Magharibi (kushoto) na Anna Lupembe wa Viti Maalum wakiwa katika Mkutano wa Wabunge wa CCM kwenye ukumbi wa Msekwa, Bungeni Mjini Dodoma Aprili 21, 2010.

 

Mbunge wa Kuteuliwa, Kingunge Ngombale-Mwiru (kulia) akiteta na Mbunge wa Bukoba Vijijini Nazir Karamagi katika mkutano wa wabunge wa CCM uliofanyika kwenye ukumbi wa Msekwa Mjini Dodoma Aprili 21, 2010.

Tuesday, April 20, 2010

 

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda , Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa na Mbunge wa Busanda, Lolesia Bukwimba (kulia) wakifurahia jambo katika mazungumzo kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Aprili 20, 2010.

 

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema (kulia) na Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa (katikati) wakiteta na Mbuge wa Sumve, Richard Ndassa , Bungeni Mjini Dodoma, Aprili 20, 2010

 

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na baadhi ya Wachimbaji madini wadogo na madiwani kutoka jimbo la Busanda wilayani Geita waliotembelea Bunge kwa mwaliko wa Mbunge wao, Lolesia Bukwimba (kulia) , kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Aprili 2010.

 

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipokea zawadi kutoka kwa Naibu Spika wa Bunge la China, Mhe. Jan Junqi katika mazungumzo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Waziri Mkuu, Bungeni Mjini Dodoma Aprili 19, 2010.

 

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Yan Junqi ambaye Aprili 20, 2010 alitembelea Bunge na baadae alikutana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwa Mazungumzo.

 

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Jan Junqi kabla ya mazungumzo yao kwenye ukumbi wa Waziri Mkuu, Bungeni Mjini Dodoma, Aprili 19, 2010.

 

Spika wa Bunge Samuel Sitta akimkabidhi zawadi, Naibu Spika wa Bunge la China, Mhe. . Jan Junqi katika chakula cha jioni alichomwandalia mgeni huyo kwenye hoteli ya Mtakatifu Gaspar Mjini Dodoma Aprili 19, 2010.

 
Wasanii wakicheza ngoma ya Hiyari ya Moyo katika chakula cha jioni alichoandaliwa Naibu Spika wa Bunge la China, Mhe. Jan Junqi kwenye hoteli ya Mtakatifu Gaspar Mjini Dodoma Aprili 19, 2010.

Monday, April 19, 2010

 

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Mbunge wa Muhambwe, Felix Kijiko (kushoto)wakitoka kwenye ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma Aprili 19,2010

 

Baadhi ya wabunge wa CCM wakiwa katika mkutano wao ulioongozwa na Mwenyekiti wa Wabunge hao, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwenye ukumbi wa Msekwa Bungeni Mjini Dodoma Aprili 18,2010

 

Mwenyekiti wa Wabunge wa CCM, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akijadili jambo na Spika wa Bunge Samuel Siitta (kulia) katika mkutano wa wabunge hao alioungoza kwenye ukumbi wa Msekwa, Bungeni Mjini Dodoma, April 18,2010.Kushoto ni Mbunge wa Peramiho na Kaimu Katibu wa Wabunge hao, Jenista Mhagama.

Sunday, April 18, 2010

 
PINDA AKAGUA UKARABATI WA RELI YA KATI


RELI ya Kati kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma na Mwanza iliyoharibiwa na mafuriko ya Desemba mwaka jana katika maeneo ya Kilosa na Mpwapwa inatarajiwa kuanza kazi tena katikati ya mwezi ujao, Waziri wa Miundombinu, Dk.Shukuru Kawambwa ametangaza leo (Jumapili Aprili 18, 2010).

Akitoa maelezo mbele ya Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda aliyekagua ukarabati wa reli hiyo eneo la Gulwe, kilomita 101 Mashariki mwa Dodoma, Dk. Kawambwa alisema sehemu kubwa ya ukarabati imekwishakamilika na matarajio ni reli kuanza kazi Mei 14 mwaka huu.

Mipango ilikuwa inaandaliwa ili usafiri wa treni za abiria kwa reli ya kati uanzie na kukamilika Dodoma ambako kati yake na Dar es Salaam yatumike mabasi, lakini Waziri Kawambwa alisema maandalizi hayo yanaweza kukutana na reli iliyokuwa tayari Mei.

Utaratibu wa mabasi hadi Dodoma baadaye treni uliwahi kutumika mwaka 1998 wakati ulipotokea uharibifu mkubwa kutokana na mafuriko, eneo la Kilosa.

Hivi sasa usafiri wa abiria kati ya Dar es Salaam na Kigoma na Mwanza ni kwa mabasi. Kwa kwenda Kigoma ni kuzunguka kupitia Kahama, mkoani Shinyanga. Kwa mizigo ni kwa malori.

Dk. Kawambwa alisema maeneo 32 ya reli hiyo yaliharibiwa baada ya mafuriko hayo ya Desemba 28 hadi 31, mwaka jana na mpaka sasa maeneo 20 yamekwishakamilika na mengine yaliyobaki yanamaliziwa, Dk Kawambwa alisema.

Baadaye Waziri Mkuu alisafiri kwa treni umbali wa kilomita 17 na kuvuka kwenye eneo lililokamilika. Katika eneo alilopita la Chibibo, reli ilikuwa imezolewa na mafuriko na kuacha gema la kina cha mita 15 na urefu wa mita 200.

Ujenzi huo ulifanywa na kikosi cha ufundi cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Kampuni ya Reli TRL, tangu Februari 5 mwaka huu kwa upande wa Mpwapwa na Februari 16 kwa upande wa Kilosa, ambako mvua ilikuwa inaendelea.

Fedha ilizoombwa kwa kazi hiyo ni zaisi ya Sh. Bilioni 15 na tayari zidi ya Sh. Bilioni 10 zimekwishatolewa na kutumika.

Siku chache baada ya mafuriko hayo, Waziri Mkuu alikagua uharibifu uliofanywa katika eneo la Gulwe na kuahidi kuwa Serikali itagharimia urejeshaji wa huduma za reli na barabara zilizoharibiwa na mafuriko katika Wilaya ya Mpwapwa, mkoani Dodoma na Kilosa, mkoani Morogoro.

Waziri Mkuu alisifia kikosi cha JWTZ kilichohusika na ujenzi kwa kufanya kazi ya uhakika na kwa haraka kuweza kuirejesha katika hali ya kawaida reli ya kati ambayo ni muhimu kwa usafiri wa abiria na mizigo nchini.

Mhe. Pinda pia alikagua ujenzi wa daraja la barabara ya Gulwe ambao umekamilika na ujenzi wa daraja la Godegode la Barabara ya kilomita 60 inayounganisha makao makuu ya Wilaya ya Mpwapwa na Godegode na Lumuma.

Ujenzi wa daraja la Godegode litakalokuwa la makalavati makubwa katika eneo la mita 100 za kuvuka mto, unatarajiwa kuanza kesho (Jumatatu Aprili 19, 2010) na kuchukua miezi miwili kwa gaharama ya Sh. milioni 774.

Waziri Mkuu ambaye alikwenda Mpwapwa kwa gari asubuhi leo (Jumapili Aprili 18, 2010) alirejea Dodoma jioni ambako anahudhuria kikao cha Bunge.

 

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua ukarabati wa reli ya kati katika eneo la Kidibo wilayani Mpwapwa Aprili 18, 2010 ambao unatarajiwa kukamilika mwezi ujao katikati na hivyo kuruhusu safari za treni kuanza.

 

Waziri Mkuu, Mizengo na Waziri wa Miundombinu, Dr. Shukuru Kawambwa (kulia) wakisafiri katika behewa la daraja la tatu kutoka stesheni ya Mpwapwa hadi Godegode wilayani Mpwapwa kwenye reli ya kati wakati alipokagua ukarabati wa reli hiyo Aprili 18, 2010 iliyoharbiwa vibaya na mafuko. Ukarabati wa reli hiyo unatarajiwa kaukamilika mwezi mei katikati na safari za treni ziataanza kama kawaida.

Saturday, April 17, 2010

 

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akihutubia katika Tamasha la Kulipongeza Bunge na Serikali kwa kupitisha sheria ya kumlinda mtoto lililofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, Aprili 17, 2010.



PINDA AHUTUBIA TAMASHA LA WATOTO LA KUUNGA MKONO BUNGE NA SERIKALI

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amelaani vikali mauaji ya kiajabu ya watoto wadogo yaliyozuka hivi karibuni katika Tarafa ya Tukuyu Wilayani Rungwe mkoani Mbeya na kuahidi kuwa Serikali itachukua hatua kali kwa wahusika watakopatikana.

Alikuwa akihutubia baada ya kupokea maandamano ya watoto kupongeza Serikali na Bunge kwa kupitisha Sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009, kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo (Jumamosi Aprili 17, 2020).

Inasikitisha kuona kuwa watoto hao wadogo wanauawa ovyo kikatili katika namna ya kutisha huku watu wazima wapo na wanashindwa kuwalinda, alisema.

Mhe. Pinda alikumbusha kuwa matukio haya ya kuua watoto wadogo yanatokea baada ya wimbi la kuwaua walemavu wa ngozi, ambao nao wengi wao wanaowindwa ni watoto wadogo pia.

“Kila nikikaa sielewi. Watanzania tufike mahali kweli turejee na kusema matendo haya siyo ya kibinadamu, hayampendezi Mungu, hasa kuwaua watoto wadogo,” alisema.

Watoto wapatao sita wameuawa kikatili huko Tukuyu hivi karibuni na Polisi imewakamata watu kadhaa wakishukiwa kuhusika na mauaji hayo ambayo yanahusishwa na imani za kichawi.

Katika hotuba yake, Waziri Mkuu alisisitiza kuwa Serikali itahakikisha kwamba Sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009 itatekelezwa kudhibiti maovu mengi yanayotendwa dhidi ya watoto.

“Napenda kutoa tahadhari kwamba kuanzia sasa tunapoanza utekelezaji wa Sheria hii, yeyote atakayebainika kuendeleza vitendo viovu kwa watoto atakuwa amegusa mboni ya jicho la Serikali.

“Adhabu kali itatolewa kwa yeyote atakayehusika na ukatili wa aina yoyote dhidi ya watoto. Kwa wale waliojenga mazoea ya kuwaonea watoto sasa waache mara moja, kwa sababu Sheria hii sasa itachukua mkondo wake," alisema.

Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009, inayozingatia upatikanaji wa haki za msingi za watoto na kuendeleza ustawi wao, inachukua nafasi ya Sheria tano ambazo zilifutwa na nyingine tano zilizofanyiwa marekebisho. Inaweka kuwa mtoto ni yule mwenye umri wa miaka 18 na kurudi chini.

Ilipitishwa na Bunge katika mkutano wa 17 Novemba mwaka jana na kuanza kufanyakazi rasmi Aprili 1, mwaka huu baada ya kutiwa saini na Mhe. Rais.

Kumekuwa na lawama nchini kuwa watoto wamekuwa wakinyimwa haki zao za msingi zikiwemo za kuishi, kupata elimu, kuendelezwa na kulindwa na kutunzwa.

Maandamano hayo yaliwashirikisha zaidi ya watoto 27,000 wa shule za Msingi na Sekondari wa Dodoma, kuwawakilisha watoto wenzao nchini kote.

 

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Spika wa Bunge, Samuel Sitta (kulia) wakifurahia zawadi walizozawadiwa na watoto wa Dodoma katika Tamasha la kulipongeza Bunge na Serikali kwa kupitisha sheria ya kumlinda mtoto lililofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma, Aprili 17, 2010. Wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. James Msekela na wanne kulia ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Margareth Sitta.

 

Watoto wa Dodoma wakipita mbele ya mgeni rasmi, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwa Maandamano katika Tamasha la Kulipongeza Bunge na Serikali kwa Kupitisha sheria ya kumlinda Mtoto kwenye uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma, Aprili 17, 2010.

 

Watoto wa Dodoma wakipita mbele ya mgeni rasmi, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwa Maandamano katika Tamasha la Kulipongeza Bunge na Serikali kwa Kupitisha sheria ya kumlinda Mtoto kwenye uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma, Aprili 17, 2010.

 

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua kazi za mikono za watoto wa Kituo cha Mlimwa Anglican kabla ya kuhutubia katika Tamasha la Kulipongeza Bunge na Serikali kwa kupitisha sheria ya kumlinda mototo lililofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma Aprili 17, 2010. Kulia ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Margareth Sitta

 

Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira (katikati) akizungumza naMWansheria Mkuu w Serikali, Jaji Frederick Werema (kulia) na Mbubge wa Musoma Mjini , Vedastus Mathayo Manyinyi kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma, Aprili 16, 2010.

Friday, April 16, 2010

 




Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Afrika ya Kusini, Radhia Msuya (katikati)na Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Patrick Tsere , Ofisini kwake Bungeni Mjini Dodoma, Aprili 16, 2010.

This page is powered by Blogger. Isn't yours?