Friday, May 21, 2010

 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Mbunge wa zamani wa Mpanda, Mzee Edward Nsalamba wakati alipokwenda kumsalimia nyumbani kwake eneo la Kashaulili Mjini Mpanda, May 17, 2010.

 

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa zamani wa Mpanda, Mzee Edward Nsalamba wakati alipokwenda kumsalimia nyumbani kwake eneo la Kashaulili Mjini Mpanda May 17, 2010. Wengine kutoka kushoto ni Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda, Mbunge wa Viti Maalum Janet Masaburi, Mbunge wa Sumbawanga Mjini , Paul Kimiti na Mbunge wa Kuteliwa na Kaimu Kamanda wa Vijana wa CCM Taifa, Kingunge Ngombale Mwiru

 

Wanachama wapya wa CCM wakiapa baada ya kukabidhiwa kadi Mpya na Mjumbe wa Kamati Kuu, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda katika Mkutano uliofanyika kwenye uwanja wa Kashaulili Mjini Mpanda , May 17, 2010.

 

Kaimu Kamanda wa Vijana wa CCM Taifa, Kingunge Ngombale Mwiru akizungumza baada ya kumtawaza, Mjumbe wa Kamati Kuu wa CCM, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuwa Kamanda wa Viajana wa CCM wa Mkoa wa Rukwa , kwenye uwanja wa Kashaulili Mjini Mpanda May 17, 2010.

 

Kaimu Kamanda wa Vijana wa CCM Taifa, Kingunge Ngombale Mwiru, Kingunge Ngombale Mwiru akimkabidhi bakora wakati alipomtawaza, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuwa Kmamanda wa Vijana wa CCM, Mkoa wa RUkwa, kwenye uwanja wa Kashaulili Mjini Mpanda Maya 17, 2010.

 

Kaimu Kamanda wa Vijana wa CCM Taifa, Kingunge Ngombale Mwiru, Kingunge Ngombale Mwiru akimtawaza, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuwa Kmamanda wa Vijana wa CCM, Mkoa wa RUkwa, kwenye uwanja wa Kashaulili Mjini Mpanda Maya 17, 2010.

 

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na MkeweTunu (kushoto) wakikagua ujezi wa Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya Mpanda wakiwa katika ziara ya wilaya hiyo, May 17, 2010.

 

Waziri Mkuu, Mkuu, Mizengo Pinda akiweka jiwe la msingi la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mpanda akiwa kaika ziara ya wilaya hiyo, May 17, 2010.

 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Mkewe Tunu (kulia ) wakipata maelezo kutoka kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Rukwa ,Isuto Damian Mantage wakati alipoweka jiwe la Msingi la Kituo cha Polisi cha wilaya ya Mpanda akiwa katika ziara ya wilaya hiyo, May 17, 2910.

 

Wasanii wa Mpanda wakitumbuiza wakati Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipoweka jiwe la Msingi la Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Mpanda akiwa katika ziara ya wilaya hiyo, May 17, 2010.

 

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipokea mchango wa Shilingi 100,000/= kutoka Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Mpanda , Thomas Ngozi zilizotokewa na wazee hao Mjini Mpanda M

 

Waziri Mkuu, Mizengo Pimda akifungua Mkutano wa Halmashauri ya CCM ya Mkoa wa Rukwa kwenye ukumbi wa CCM wilaya ya Mpanda May 16, 2010 . Kulia ni Mkewe Tunu na kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Rukwa, Hypolitus Matete na wapili kulia ni Kamu Mkuu wa Mkoa wa Rukwa na Mkuu wa wilaya ya Sumbawanga, Kanali Antonio Mzurikwao.

 

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwapungia wananchi wa Kijiji cha Mtapenda wilayani Mpanda wakati alipowasili kijijini hapo kuhutubia mkutano wa hadhara akiwa katika ziara ya wilaya hiyo, May 15, 2010. Kushoto kwake ni mkewe Tunu.

 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwapungia wananchi wa Kijiji cha Mtapenda wilayani Mpanda wakati alipowasili kijijini hapo kuhutubia mkutano wa hadhara akiwa katika ziara ya wilaya hiyo, May 15, 2010. Kushoto kwake ni mkewe Tunu.

 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua ubora wa tumbaku nchini wakati alipozindua Msimu wa Uuzaji tumbaku katika kijiji cha Majalila wilayani Mpanda May 13, 2010. Kulia ni Mkewe

 
KILIMO CHA JEMBE LA MKONO SASA BASI - PINDA

Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda amesema Kilimo cha Jembe la Mkono Nchini sasa basi kwa vile kimeshindwa kuleta Mapinduzi ya Kilimo na badala yake lazima kutumia zana za Kisasa na Utalaamu.

Alikuwa akihutubia Mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Mirumba, Kata ya Kibaoni, Tarafa ya Mpimbwe baada ya kukabidhi Matrekta kwa vikundi vya Wakulima katika siku yake ya nne ya ziara yake ya Jimbo.

“Jembe la Mkono siyo zana ya kutegemea kubadili maisha yetu… Wenzetu wanalima kwa Matrekata madogo na makubwa, wanapanda na kuvuna kwa Matrekta… Majembe ya Mkono yalitumika zaidi ya Miaka 2000 iliyopita” alisema.

Alikabidhi Trekta moja kubwa kwa kikundi cha Mbugani cha Kijiji cha Itenka; moja dogo kwa kikundi cha Jitume cha Kijiji cha Magamba na jingine dogo kwa kikundi cha Ufugaji Nyuki cha Kijiji cha Uruira.

Trekta kubwa aina ya Tafe, liliotengenezwa India, lina thamani ya Shilingi Milioni 51 na Wakulima wanatakiwa kuilipa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Shilingi Milioni 10 ambayo ni Asilimia 20 ya gharama Halmashauri hiyo iliingia kulinunua.

Trekta dogo aina ya Kubota la Japan Wakulima hutakiwa kulipia Shilingi Milioni 1.5, ikiwa ni Asilimia 10 tu ya bei yake.

Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda tangu mwaka 2007/2008 imekuwa ikitekeleza agizo la Serikali la kununua Matrekta na kuyasambaza kwa Wakulima kwa bei ya chini, ikiwa ni sehemu ya kuendeleza Kilimo cha zana na cha Kisasa.

Kwa mwaka huu wa fedha unaomalizika Mwezi ujao (2009/2010), Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda ilipanga kununua Matrekta madogo 36, kwa gharama ya Shilingi Milioni 284 na Matrekta makubwa matano ya Shilingi Milioni 258, ikiwa ni utekelezaji wa Mpango huo.

Matrekta madogo 11 yaliyogharmu Shilingi Milioni 78 yaligawiwa kwa vikundi 11 vya Tarafa za Nsimbo, Karema, Mpimbwe na Kabungu, kwa mwaka 2008/2009.

Trekta kubwa kwa saa 8 kwa kutwa hulima kiasi cha ekati 10 na dogo ekari 5 wakati kwa Mkono, kwa Mkulima mmoja hata eka moja haiwezekani kuilima kwa kutwa nzima, kwa mujibu wa Wataalamu.

Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda pia imenunua Mashine ya Kisasa ya kukobolea Mpunga na kuupanga Mchele kwa Madaraja, kwa gharama ya Shilingi Milioni 250 ili kuongeza thamani ya zao hilo na kuongeza pato la Mkulima.

Mashine hiyo ya kutoa Mchele, itawekwa katika Kijiji cha Mwamapuli kwenye Soko kubwa la Kisasa lililojengwa na Halmashauri kuptia mpango wake maendeleo wa Wilaya kuwaendeleza Wakulima.

Mheshimiwa Pinda pia alikabidhiwa michango ya Wananchi mbalimbali waliojitolea kumlipia fomu ya kugombea Ubunge kupitia kwa Chama chake cha CCM, uliofikia Shilingi 305,000/= katika Kijiji cha Mirumba; Shilingi zaidi ya 102,300/=, katika Kijiji cha Itenka ‘B’ (zikiwemo 2,000/=) zilizochangwa na Mlemavu na Shilingi 300/= za Mtoto wa Shule) na Shilingi 10,000/= katika Kijiji cha Kasansa.

Gharama za fomu ni Shilingi 100,000/= na Mheshimiwa Pinda alizikabidhi fedha zilizosalia kwa CCM, Wilaya ya Mpanda kwa matumizi ya CCM na Jumuiya zake kwa shughuli za Kichama.

Kabla ya kuwasili Mpanda Mjini leo (Jumanne Mei 11, 2010) Waziri Mkuualitembelea Kijiji cha Itenka B na kuzungumza na Wananchi katika Mkutano wa hadhara.

Jana (Jumatatu Mei 10, 2010), alitembelea Kasansa, Kanindi ambako alikuwa na mikutano ya hadhara na kuhimiza Kilimo na akatembelea Majimoto ambako alikagua Jengo la Kisasa la SACCOS (Chama cha Kuweka na Kukopa) ya Majimoto, ambayo ni Makao Makuu ya Kata ya Majimoto katika Tarafa ya Mpimbwe.

Waziri Mkuu aliwasili Mpanda Jumamosi (Mei 8, 2010) na Jumapili akazungumza na Wananchi wa Kijiji cha Kibaoni, waliokubaliana kuanzisha Kilimo cha bega kwa bega kwa kutumia Trekta kubwa.

Kesho (Jumatano Mei 12, 2010) atatembelea Kamsisi na Mtakuja ambako atakuwa na Mkutano wa hadhara.

Anatarajiwa kurejea Dar es Salaam Mei 18, 2010 baada ya ziara yake ya Jimbo.

 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Bibi Maria Katyega (kulia) wa kijiji cha Ulwira Misheni akiwa katika ziara ya wilaya ya Mpanda May 12, 2010.

 

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Mkewe Tunu wakifurahia baada ya Waziri Mkuu kutawazwa kuwa mtemi wa Wakonongokatika mkutano wa hadhara aliouhutubia kwenye kijiji cha Kamsisi wilayani Mpanda May 12, 2010. Katikati ni Mweyekiti wa Halmashauri ya wiIaya ya Mpanda, Philip Kaliyaya,

 


Msanii Michael Kapepe wa kikundi cha ngoma ya asili ya Uyeye cha kijiji cha Kanoge wilayani Mpanda akcheza ngoma hiyo akiwa na joka katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu kwenye kijiji cha Kamsisi, May 12, 2010.

 

Msanii Michael Kapepe wa kikundi cha ngoma ya asili ya Uyeye cha kijiji cha Kanoge wilayani Mpanda akcheza ngoma hiyo akiwa na joka katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu kwenye kijiji cha Kamsisi, May 12, 2010.

 

Mpiga ngoma akitumbuiza katika Mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu , Mizengo Pinda kwenye kijiji cha Kamsisi wilayani Mpanda May 12, 2010.

 

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiendesha Trekta kubwa kabla ya kulikabidhi kwa Kikundi cha Kilimo Kwanza Usevya wilayani Mpanda ambacho kimelinunua kikisaidiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda , Trekta hilo limeuzwa kwa kikundi hicho na kampui ya Farm Equip (TANZANIA) Company Limited

 

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimshukuru mtoto Anthony Daniel (7) wa Darasa la saba katika shule ya Msingi ya Intenka wilayani Mpanda baada ya kukabidhiwa shilingi 300/= ukiwa ni mchango wa kumwezesha Waziri Mkuu kuchukuwa Fomu za kuwania ubunge katika jimbo la Uchaguzi la Mpanda Mashariki jwenye uchaguzi mkuu ujao. Alikuwa akihutubia Mkutano wa hadhara katika kijiji cha Itenka wilayani humo

 

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Mkewe Tunu wakikagua jengo la SACCOS ya Majimoto wilayni Mpanda wakiwa katika ziara ya wilaya hiyo May 10, 2010.

 

Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Mkewe Tunu (kushoto) wakizungumza na wachama wa Chama cha Kuweka na Kukopa (SACCOS) cha MajiMoto wakati walipotembelea ofisi za SACCOS hiyo wilayani Mpanda wakiwa katika ziara ya wilaya hiyo, May 10, 2010.

 

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Polisi Fare ambaye ni Mfugani Mfugaji wa Kijiji cha Ikulwe wilayani MPanda baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Kanindi, May 10, 2010. Katikati ni mkewe Tunu.

 

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimkabidhi mkewe Tunu (kulia) zawadi ya jogoo aliyopewa na wanakijiji cha Kasansa wilayani Mpanda akiwa katika ziara ya wilaya hiyo, May 10, 2010. Katikati ni Mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo, Sebastian Kapufi.

 

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizunguma na Bi. Anna Funta wa kijiji cha Kibaoni wilayani Mpanda akiwa katika ziara ya wilaya hiyo, May 9, 2010.

 

Waziri Mkuu, Mizengo PInda akizungumza na Wakulima wa Kijiji cha Kibaoni wilayani Mpanda akiwa katika ziara ya wilaya ya Mpanda May 9, 2010

 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Mkewe Tunu wakipokewa na wananchi wa kijiji cha Kibaoni wilayani mpanda baada ya kuwasili kijijni hapo May 10, 2010 wakiwa katika ziara ya wilaya ya Mpanda.

Tuesday, May 18, 2010

 

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Viongozi wa Tanganyika Law Society, Ofisini kwake jijini Dar es salaam May 7, 2010.

 

Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kilosa , Halima Dendego mchango wa Shilingi milioni sita zikiwa ni mchango wa wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu kwa ajili ya wanachi wa wilaya hiyo waliokumbwa na mafa ya mafuriko. Katika makabidhiano hayo yaliyofanyika kwnye makazi ya Waziri Mkuu jijijni Dar es salaam May 7, 2010,Mama Pinda pia alilabidhi nguo, sabuni na viatu.

 

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Rais wa Namibia Hifikepunye Pohamba katika chakula cha usiku kilchoandaliwa na Rais Jakaya Kiwete Ikulu jijini Dar es salaam kwa ajili ya Viongozi na Washiriki wa Mkurutano wa Uchumi, May 6, 2010.

 

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula Duniani (WFP), Bi. Sheila Sisula kabla ya mazungumzo yao, Ofisi ni kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam, May 6, 2010.

 

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mwenyekiti wa Serengeti Breweries, Mark Bomani (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya East African Breweries, Seni Adetu , Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam May 5, 2010.

 

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Mwenyekiti wa Serengeti Breweries, Mark Bomani (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya East African Breweries, Seni Adetu kabla ya mazungumzo yao, Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam May 5, 2010.

 


 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya East African Breweries, Seni Adetu kabla ya mazungumzo yao, Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam May 5, 2010.

 

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiongozana na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika, Bi. Obiageli Ezekwesili kutoka kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Dar es salaam baada ya kufunga mkutano wa Uwekezaji aliouitisha na kuungoza kwenye ukumbi huo May 6, 2010. Kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo.

 

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia, Kanda ya Afrika, Bi. Obiageli Ezekwesili katika Mkutano wa Uwekezaji nchini aliouitisha na kuuongoza kwenye ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es s alaam May 6, 2010.

 

Waziri wa Zamani wa Uingereza, Bi. Lynda Chalker akichangia katika Mkutano wa Uwekezaji nchini ulioitishwa na kuongozwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwenye ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania jijini Da es salaam May 6, 2010.

 

Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika , Bi. Obiageli Ezekwesili akizungumza katika Mkutano wa Uwekezaji nchini ulioitishwa na kuongozwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwenye ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es salaam, May 6, 2010.

Wednesday, May 05, 2010

 

Mkuu, Mizengo Pinda akiagana na Waziri Mkuu wa Zimbabwe, Morgan Tsavangirai baada ya mazungumzo yao, Ofisi ni kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam May 5, 2010.

 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiagana na Waziri Mkuu wa Zimbabwe, Morgan Tsavangirai baada ya mazungumzo yao, Ofisi ni kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam May 5, 2010.

 

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Waziri Mkuu wa Zimbabwe, Morgan Tsavangirai, Ofisini kwake jijini Dar es salaam May 5, 2010. Tsavangirai yuko nchini kuhudhuria mkutano wa Uchumi

 
AL-SHAYMAA, KIMAYA WATANGAZA NIA KUWANIA UBUNGE MBELE YA WAZIRI MKUU

MBUNGE wa Kuteuliwa na Rais, Bi. Al-Shaymar John Kwegyir na Mwenyekiti wa Chama cha Watu Wenye Ulemavu wa Ngozi Tanzania, Bw. Ernest Kimaya ambao wote ni walemavu wa ngozi wametangaza nia ya kugombea ubunge katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba, mwaka huu.

Akizungumza na wakazi wa mji wa Iringa, leo mchana (Jumanne, Mei 04, 2010) wakati wa maadhimisho ya Siku ya Walemavu wa Ngozi Tanzania yaliyofanyika kwenye viwanja vya Garden mjini humo, Bw. Kimaya amesema ana nia ya kugombea ubunge jimbo la Korogwe Vijijini kwa tiketi ya CCM.

Alisema amefikia uamuzi huo ili kitimiza kauli mbiu ya mwaka huu ambayo inawahimiza wajitokeze kugombea. Kaulimbiu ya mwaka huu inasema: “Uchaguzi wa Serikali, Mlemavu wa Ngozi ana Haki ya Kuchagua na Kuchaguliwa, Tujitokeze”.

Akihutubia wakazi hao, Waziri Mkuu Mizengo Pinda alisema amedokezwa na mbunge Kwegyir kwamba ana nia ya kwenda kugombea viti maalum mkoa wa Tanga. “Anasema anamshukuru Rais Kikwete kumteua katika ubunge na sasa anataka aende viti maalum,” alisema Waziri Mkuu.

“Napenda kutoa wito kwa wananchi wote wakiwemo watu wenye Ulemavu wa Ngozi nchini kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali kupitia vyama vyao vya siasa, mnayo fursa ya kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kama ilivyo kwa wananchi wengine. Jitokezeni pia kwenye zoezi zima la upigaji kura. Wote mnayo haki ya msingi kushiriki kikamilifu katika zoezi hili kama ilivyo kwa Watanzania wote,” alisema.

Aliwataka Watanzania watambue kuwa watu wenye ulemavu wa ngozi wana mchango mkubwa katika jamii hasa wakiwezeshwa na binadamu wenzao wasio na ulemavu huo. “Wito wangu kwa jamii ya Watanzania ni kuwa Iwape Nafasi Kwani Wanaweza,” alisema.

Maadhimisho hayo pia yalihudhuriwa wa wawakilishi wa watu wenye ulemavu kutoka mikoa zaidi 15, Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Aisha Kigoda; Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Bw. Mohammed Abdulaziz; Mbunge Kwegyir; Bi. Margareth Mkanga na wabunge wengine kutoka mkoa wa Iringa.

 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Askofu wa Jimbo Katoliki la Iringa Mhashamu, Tarcisius Ngalalekumtwa katika maadhimisho ya Siku ya Walemavu wa Ngozi Tanzania yaliyohutubiwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwenye viwanja vya Garden Mjini Iringa May 4, 2010

 
WAUZA VIUNGO VYA WALEMAVU SIKU ZENU ZINAHESABIKA - PINDA

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda ametoa onyo kwa watu wanaojihusisha na vitendo vya ukataji viungo vya watu wenye ulemavu wa ngozi waache kufanya hivyo mara moja kwa sababu siku zao zinahesabika.

“Napenda kuwaonya watu wote wanaojihusisha na vitendo viovu vya ukataji wa viungo na wauaji wa walemavu wa ngozi popote walipo kuwa siku zao zinahesabika. Ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi nawahakikishia Serikali itashinda vita hii na mtaishi kwa uhuru ndani ya nchi yenu,” alisema.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumanne, Mei 04, 2010) wakati akiwahutubia wakazi wa mji wa Iringa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Walemavu wa Ngozi Tanzania yaliyofanyika kwenye viwanja vya Garden, mjini humo.

Alisema Serikali itafanya kila liwezekanalo kuhakikisha inatokomeza ukatili na unyama wa aina yoyote wanaofanyiwa wananchi wenye ulemavu wa ngozi. Alitumia fursa hiyo pia kuwaonya waganga wa kienyeji waache kuchochea ukatili huo kwa kuwadanganya watu.

“Nawaomba viongozi wa dini na taasisi zisizo za kiserikali waendelee kuwaelimisha Watanzania juu ya vitendo hivi viovu, vinavyofanywa na wauaji hawa. Ninawasihi waganga wa kienyeji waache kutumika kuchochea ukatili huo. Wasiwadanganye watu kwani hakuna utajiri unaopatikana kwa kukata mkono wa binadamu mwenzako... utajiri unapatikana kwa juhudi zako siyo kwa kuua,” alisisitiza.

Alisema pamoja na kuwa nchi inaadhimisha siku hiyo ya walemavu wa ngozi, bado Serikali inakabilwia na changamoto ya kukabili matukio ya mauaji ya walemavu hao nchini ambapo alibainisha kuwa tangu Oktoba mwaka jana hadi sasa, mlemavu mmoja wa ngozi ameuawa na wengine watatu wamejeruhiwa. Hata hivyo, Waziri Mkuu alisema hali imetulia ikilinganishwa na miata mitatu iliyopita.

Akichanganua takwimu za kura ya maoni iliyofanyika nchini nzima Machi mwaka jana, Waziri Mkuu alisema jumla ya watu 97,736 walipigiwa kura kuwa wanahusika na makosa mbalimbali yakiwemo ya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi na kwamba upelelezi wa kina unaendelea kuhusu watuhumiwa hao.

Akifafanua zaidi alisema: “Hadi sasa, watu 3,217 wamefikishwa polisi, watu 295 wamefikishwa mahakamani ambapo kati yao, watu 106 wamehukumiwa kwa makosa mbalimbali, yakiwemo ya vitendo vya ukatili dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi.”

“Kati ya kesi zilizofikishwa mahakamani, 11 ni za mauaji ya walemavu wa ngozi. Kesi tatu zimetolewa hukumu na watuhumiwa wanane wamehukumiwa kifo. Upelelezi wa matukio mengine 27 ya mauaji unaendelea,” aliongeza.

Akizungumzia kuhusu maombi yao ya kupewa upendeleo wa kupata mikopo kwenye mabenki, Waziri Mkuu alisema sio rahisi kuyaagiza mabenki yaweke masharti nafuu kwa ajili ya walemavu wa ngozi pekee yao kwa kuwa huduma hiyo hutolewa kwa uwiano na biashara ya sasa ni huria.

“Nawashauri mjiunge kwenye SACCOS ili muweze kupata mikopo kwa ajili ya uzalishaji mali muweze kujikwamua kiuchumi. Mkiweza vile vile muendeleze mshikamano miongoni mwenu na mtumie fursa hiyo kujenga SACCOS yenye nguvu… mtaweza kupata fursa za kupata mitaji kama vile Mabilioni ya JK kwa manufaa yenu na ya jamii yote ya watu wenye ulemavu kwa ujumla,” alisema.

Aliwataka Watanzania watambue kuwa watu wenye ulemavu wa ngozi wana mchango mkubwa katika jamii hasa wakiwezeshwa na binadamu wenzao wasio na ulemavu huo. “Wito wangu kwa jamii ya Watanzania ni kuwa Iwape Nafasi Kwani Wanaweza,” alisema.

 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akihutubia katika Maadhimisho ya Siku ya Walemavu wa Ngozi Tanzania kwenye viwanja vya Garden Mjini Iringa May 4, 2010. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Walemavu Tanzania, Ernest Kimaya

 

Wasanii, Fadhili Kambi wa kikundi cha Albino Revolution (kushoto) na Mwasiti Mativira wa ndi cha Hisia Cultural Goup wakiingiza igizo la mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi yaani albino katika maadhimisho ya siku ya walemavu wa ngozi Tanzania kwenye viwanja vya Garden Mjini Iringa May 4, 2010. Mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda

 

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Waandishi wa Habari May 2, 2010 baada ya kukagua maadalizi ya mapokezi ya wageni watakaoshiriki katika Mkutano wa World Economic Forum unaotarajiwa kufanyika jijini Dar es salaam kuanza May 5, 2010 kwenye ukumbi wa Mlimani City utakapofanyia mkutano huo. Kulia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Peniel Lymo na kushoto ni Mkurugenzi wa Afrika wa World Economic Forum, Catherine Tweedie.

 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na mafundi na wahandisi wa Kichina wanaojenga jengo la mapokezi la viongozi na watu mashuhuri kwenye uwanja wa dege wa Julius Nyerere May 2, 2010 ambalo litatumika katika mapokezi ya viongozi watakaowasili nchini kuhudhuruia mkutano wa World Economic Forum unaotarajiwa kuanza kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar e salaam, May 5, 2010.

 

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua maandalizi ya mapokezi ya viongozi wakuu wa n chi mbalimbali na washiriki wa Mkutano wa World Economic Forum kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere May 2, 2010. Mheshimiwa Pinda pia alikagua ukumbi wa Mlimani City utakapofanyika mkutano huo

 

Jengo la maabara ya hospitali ya mkoa wa Singida lililozinduliwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda Aprili 30, 2010

 
SERIKALI KUSAIDIA UJENZI WA HOSPITALI YA RUFANI SINGIDA - PINDA

Sigida, may 1, 2010

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema Serikali itatafuta njia za kusaidia ujenzi wa hospitali ya Rufaa ya Singida ili iweze kukamilika haraka badala ya kusubiri sh. bilioni mbili za bajeti ya mkoa zinazotolewa na Serikali kuu kila mwaka.

Amesema kukamilika kwa ujenzi wa hospitali hiyo itakayogharimu sh. bilioni 80 kutakuwa na manufaa zaidi kwani kutaifanya iweze kuhudumia kanda ya kati ambayo haijawahi kuwa na hospitali ya rufaa tangu nchi ipate uhuru.

Ametoa kauli hiyo jana jioni (Ijumaa, Aprili 30, 2010) wakati akihutubia wakazi wa mji wa Singida katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa michezo wa Namfua, mjini Singida.

“Ukienda Tabora hakuna hospitali ya rufaa, Dodoma na Shinyanga nako hakuna. Manyara ndiyo kwanza wameanza kujenga hospitali yao ya mkoa… kwa hiyo hii hospitali yenu ni tegemeo la kanda ya kati yote,” alisema.

Waziri Mkuu ambaye alikuwa katika siku ya nne ya ziara yake ya siku tano mkoani hapa, alisema uzuri wa hospitali hiyo unasababishwa ukweli kwamba vifaa vya kutoa huduma vimekwishawasili ikiwa ni msaada kutoka Marekani.

Alisema hospitali ya sasa ilijengwa mwaka 1954 wakati huo mkoa wa Singida ukiwa na wakazi 300,000 tu lakini sasa ni zaidi ya milioni moja. Kwa hiyo imelazimu miundombinu iongezeke na hospitali hiyo ya rufaa itaiokoa hiyo ya mkoa.

Mapema jana mchana, Waziri Mkuu alitembelea hospitali hiyo iliyoko kata ya Mandewa katika Manispaa ya Singida na kuweka jiwe la msingi katika majengo ya wagonjwa wa nje na wodi ya wazazi.

Alisifu juhudi za mkoa huo kwa kuwa na idadi ndogo ya vifo vya wanawake wajawazito ambapo mkoa huo takwimu zaker zinaonyesha kuwa mwaka 2005 kulikuwa na vifo 233 kwa kila akinamama 100,000 waliokuwa wanajifungua ikilinganishwa na takwimu za kitaifa mabzo zilikuwa ni vifo 578 kwa akila akinamama 100,000 waliokuwa wanajifungua.

“Hivi sasa idadi imeshuka kutoka 233 na kufikia 119 ... hii ni kwa takwimu za mwaka jana 2009, hili limenifariji sana kwani inadhihirisha kuwa akinamama wa Singida wanakwenda kujifungulia kwenye zahanati na vituo vya afya. Mmenipa faraja kuwa hili tatizo linaweza kuisha kabisa hapa nchini, kama tukidhamiria kuliondoa,” alisema.

Alisema takwimu zimeshuka pia katika idadi ya vifo vya watoto walio chini ya umri wa miaka mitano na kwamba mkoa umefanya vizuri katika usambazaji wa vyandarua ili kukabiliana na tatizo la malaria.

Leo asubuhi (Jumamosi, Mei Mosi 2010), Waziri Mkuu atafanya majumuisho ya ziara yake katika mkoa huo kwenye ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi (FDC) Singida na kisha kuelekea Dodoma akiwa njiani kurejea jijini Dar es Salaam.

 

 

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akifungua jengo la Wodi ya Macho katika hospitali ya Mkoa wa Singida akiwa katika ziara ya mkoa huo Aprili 30, 2010. Kushoto ni Mkewe Tunu na kulia ni Mbunge wa Singida Mjini Muhammed Dewji.

 


This page is powered by Blogger. Isn't yours?